Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan Sadiq al-Mahdi afariki dunia
2020-11-26 18:31:33| CRI

Waziri Mkuu wa zamani wa Sudan na kiongozi wa Chama cha National Umma NUP Sadiq al-Mahdi amefariki dunia kwa virusi vya Corona, akiwa na umri wa miaka 84.

Kwa mujibu wa taarifa ya NUP, Al-Mahdi alisafirishwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu ili kupatiwa matibabu baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na COVID-19 mapema mwezi huu, lakini hali yake ilikuwa mbaya zaidi katika saa za mwisho na kufariki na nimonia kali iliyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Al-Mahdi aliyezaliwa Disemba 1935 katika mji wa Omdurman nchini Sudan, alitumikia kama waziri mkuu wa nchi hiyo kwa mwaka mmoja katika mwaka 1966 hadi 1967 na baadaye kutumikia tena katika mwaka 1986 hadi 1989.