TUZO: FIFA latoa orodha ya wanasoka 11 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia 2020
2020-11-26 18:32:50| cri

Shirikisho la soka Duniani (FIFA), limetoa orodha ya wanasoka 11 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Dunia 2020, tuzo hiyo itatolewa Disemba 17, 2020, sambamba na tuzo ya kocha bora, wa kike na wakiume, golikipa bora na goli bora la mwaka. Katika orodha hiyo mabingwa wa England klabu ya Liverpool ndio imeongoza kwa kutoa wachezaji wengi, imetoa wachezaji 4 ambao ni Thiago Alcântara, Sadio Mané, Mohamed Salah, na Virgil van Dijk. Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo, Kevin De Bruyne, Robert Lewandowski, Kylian Mbappé, Lionel Messi, Neymar, na Sergio Ramos . Mwaka jana 2019 tuzo hii alishinda mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Makocha wanaowania tuzo ya kocha bora ni Marcelo Bielsa wa Leeds United FC, Hans- Flick wa FC Bayern München, Jürgen Klopp Liverpool FC, Julen Lopetegui wa Sevilla FC na Zinedine Zidane waReal Madrid CF.