Uganda yazindua mkakati wa kuchunguza COVID-19 nyumba kwa nyumba
2020-11-26 19:06:53| CRI

Uganda imepitisha mkakati wa Timu ya Afya Kijijini VHT kama njia mpya kupambana na wimbi jipya la virusi vya Corona nchini.

Chini ya mkakati wa VHT, wanajamii ambao wana ujuzi wa msingi kuhusu huduma za afya wanakwenda nyumba kwa nyumba kuangalia hali ya afya ya wenyeji. Anapogunduliwa mtu wanayemhisi ana COVID-19, atapelekwa katika kituo cha karibu cha afya kupimwa zaidi. Wajumbe wa VHT pia watatoa elimu kwenye kila kaya kuhusu kufuata kanuni ya umbali wa kijamii na masuala ya afya ili kuepuka kuambukizwa COVID-19.

Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya, Uganda imeandikisha wagonjwa wapya 484 wa COVID-19 jana Jumatano, na kufanya idadi ya jumla kuwa 18,890. Wakati huohuo, vifo vipya vitano viliripotiwa nchi nzima, na idadi ya jumla kufikia 191.