Tanzania yawaonya waangalizi wa misitu na wanyamapori dhidi ya kula njama na wawindaji haramu
2020-11-26 09:26:02| CRI

Mamlaka nchini Tanzania imewaonya wahifadhi wa misitu na wanyamapori katika hifadhi za taifa nchini humo na wanyamapori dhidi ya kula njama na wawindaji haramu.

Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo Allan Kijazi amesema, wahifadhi wanaohusishwa na kula njama na wawindaji haramu watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kufutwa kazi. Amesema wahifadhi wa misitu na wanyamapori wanatakiwa kuongoza katika kampeni dhidi ya uwindaji haramu badala ya kushirikiana na wawindaji haramu.