Wanasayansi nchini Kenya wakimbizana na muda kuendeleza mbegu za kisasa zinazohimili mabadiliko ya tabianchi
2020-11-26 09:26:34| CRI

Kituo cha Utafiti wa Kilimo na Mifugo nchini Kenya (KALRO) kilichoko Kibos, magharibi mwa Kenya kinafanya utafiti wa mbegu za kisasa zitakazohimili mabadiliko ya tabianchi.

Katika kituo hicho, mamia ya miche ya mahindi imepanda, mingine ikiwa imeathiriwa sana na wadudu na mingine ikiwa salama. Kituo hicho ni tumaini la Kenya la kuongeza mavuno ya mahindi na kupata mbegu ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na pia zenye kinga dhidi ya wadudu na magonjwa, na pia zinazoweza kuongeza mavuno.

Mtafiti na mkurugenzi wa Kituo hicho Crispin Omondi amesema, wanatumia mbegu mpya ili kupunguza gharama za uzalishaji, kupunguza magonjwa na pia kuongeza mavuno. Ameongeza kuwa, majaribio yao yameonyesha kuwa mbegu za sasa za mahindi zilizoko sokoni haziwezi kuzuia wadudu na magonjwa, hivyo wakulima kutumia gharama kubwa kuokoa mazao yao, na hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.