Nyota wa soka Diego Maradona afariki akiwa na umri wa miaka 60
2020-11-26 09:11:02| CRI

Mchezaji bora zaidi wa soka duniani Diego Maradona aliyeongoza timu ya taifa ya Argentina kupata ubingwa wa kombe la dunia la mwaka 1986, amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 60. Ikulu ya Argentina imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kutokana na kifo hicho. Rais wa nchi hiyo Alberto Fernandez ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii akisema, Maradona aliifikisha nchi hiyo katika kilele cha dunia, na kwamba atakumbukwa daima.