Maonyesho ya Uuzaji Nje ya Shandong yafunguliwa nchini Kenya
2020-11-27 08:55:17| CRI

Maonyesho ya tatu ya Uagizaji Bidhaa Nje ya Shandong yamefunguliwa jijini Nairobi, Kenya, huku kampuni zaidi ya 93 za China zikionyesha bidhaa zao za ubora wa juu.

Kwa mujibu wa waandaaji wa maonyesho hayo, Afripeak Expo Kenya, maonyesho hayo ya biashara yanatarajiwa kuvutia wajumbe 2,100 watakaoshiriki moja kwa moja ama kupitia mtandao.

Mkurugenzi wa Afripeak Expo Kenya Gai Wei amesema, maonyesho hayo yameendelea kuwa makubwa na sio tu ni maonyesho ya biashara bali pia ni jukwaa la mawasiliano ya kibiashara na kuvutia uwekezaji wa kigeni.

Naye Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Kenya (KenInvest) Pius Rotich amesema, maonyesho hayo ni moja ya majukwaa kwa ajili ya China kujenga mtindo mpya wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Afrika, hususan Kenya.