Watu wasiopungua 40 wakwama baada ya mgodi kuporomoka Zimbabwe
2020-11-27 17:03:15| cri

Wachimba migodi wasiopungua 40 wamekwama baada ya mgodi kuporomoka kaskazini mashariki mwa Zimbabwe. Shirikisho la madini nchini humo limesema ajali hiyo ilitokea katika mji wa Bindura ulioko kilomita 70 kaskazini mwa mji mkuu wa Harare. Mkuu wa shirikisho hilo la madini Wellington Takavarasha amesema juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao bado zinaendelea. Hata hivyo serikali imesema idadi kamili ya waliokwama bado haijajulikana.Hadi kufikia sasa ni wachimbaji 6 pekee ambao wameokolewa. Mgodi huo unaojulikana kama Ran ulifungwa miaka 10 iliyopita lakini watu bado wanaonekana wakiendesha shughuli za uchimbaji madini kutafuta riziki.