Namibia yasaini mpango wa kimataifa wa chanjo ya virusi vya Corona COVAX
2020-11-27 19:57:14| CRI

Naibu katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Utafiti na Mahusiano ya Umma nchini Namibia Ben Nangombe amesema, Namibia imeidhinisha malipo ya kwanza ya dola za Namibia milioni 26.4 ikiwa ni sawa na dola milioni 1.7 za kimarekani, kwa ajili ya mpango wa kimataifa wa chanjo ya COVID-19 ya COVAX.

Nangombe amesema kuwa, Namibia italipa fedha hizo wiki ijayo, na kuiwezesha nchi hiyo kupata chanjo ya virusi vya Corona kwa asilimia 20 ya watu wake.