Kampuni ya StarTimes ya China yatangaza mkataba wa matangazo na Shirikisho la Soka la Kenya
2020-11-27 08:57:26| CRI

Kampuni ya televisheni ya kulipia ya China StarTimes imekuwa mwenzi rasmi wa matangazo wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) baada ya kusaini mkataba wa miaka saba wenye thamani ya shilingi milioni 110 za Kenya kwa mwaka. Mkataba huo mpya ni pamoja na kutangaza mechi za Ligi Kuu na mechi za Ligi Daraja la Kwanza za Kenya, pamoja na mechi za kirafiki za timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.