Sudan yasema maslahi ya taifa ni sababu pekee ya kujiunga na mazungumzo kuhusu bwawa la Mto Nile la Ethiopia
2020-11-27 09:03:39| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan amesema maslahi ya kitaifa ya Sudan yatakuwa sababu pekee ya nchi hiyo kujiunga na mazungumzo kuhusu Bwawa la Grand Renaissance la Ethiopia (GERD).

Bw. Al-Burhan amesema, anaunga mkono uamuzi uliotolewa na ujumbe wa nchi hiyo wa kutoshiriki mazungumzo ya pande tatu juu ya GERD yaliyopangwa kufanyika Novemba 21.

Sudan inataka wataalam wa Umoja wa Afrika wapewe nafasi kubwa zaidi ili kupunguza tofauti ya maoni kati ya nchi tatu zinazohusika.