Kinu cha kwanza cha umeme wa nyuklia cha Fuqing chaunganishwa kwenye gridi
2020-11-27 17:06:10| CRI

Kinu cha kwanza cha umeme wa nyuklia cha Fuqing chaunganishwa kwenye gridi

Kinu cha kwanza cha umeme wa nyuklia kinachotumia teknolojia ya Hualong One, ambao ni usanifu wa kizazi cha tatu ulioendelezwa na China, kimeunganishwa kwenye gridi usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Nyuklia la China CNNC, kinu namba 5 cha umeme wa nyuklia cha mjini Fuqing, mkoani Fujian mashariki mwa China, kiliunganishwa kwenye mtandao wa umeme saa 6:41 usiku na kuanza kuzalisha umeme.

Meneja mkuu wa Shirika la umeme wa Nyuklia la Fuqing Fujian, amesema kinu hicho kinafanya kazi vizuri, ambapo utendaji wa kiteknolojia umefikia mahitaji ya usanifu wake, pia kitafanyiwa majaribio mfululizo kabla kuanza shughuli zake kibiashara. Amesema kuunganishwa kwa mafanikio kwa kinu hicho kutasaidia kuimarisha ushindani wa sekta ya umeme wa nyuklia ya China, kuboresha muundo wa umeme wa nchi na kuhimiza maendeleo yasiyo na uchafuzi na kaboni chache.