Zimbabwe yazindua gari linalotumia umeme kuharakisha matumizi ya nishati safi
2020-11-27 08:57:04| CRI

Zimbabwe imezindua gari linalotumia nishati ya umeme wakati nchi hiyo ikijitayarisha kubadilisha magari ya mafuta yanayotumiwa hivi sasa kuwa magari yanayotumia nishati safi. Waziri wa maendeleo ya nishati wa nchi hiyo Bw. Zhemu Soda amesema hatua ya matumizi ya teknolojia ya gari linalotumia umeme inaendana na mustakabali wa kuwa nchi ya kisasa na ya kiviwanda itakapofika mwaka 2030. Ameongeza kuwa magari yanayotumia nishati ya umeme yatakuwa nguvu itakayoleta mabadiliko katika sekta ya nishati, mfumo wa uchukuzi, na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.