Rais wa sasa wa Burkina Faso ashinda katika uchaguzi mkuu
2020-11-27 08:56:38| CRI

Matokeo ya awali yaliyotolewa jana na Tume ya Uchaguzi ya nchini Burkina Faso yameonesha kuwa, rais wa sasa o Roch Marc Christian Kabore amepata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 22 mwezi huu, na kujihakikishia muhula wa pili katika washifa huo. Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Christian ameahidi kuongeza juhudi zaidi katika kujenga Burkina Faso kuwa nchi yenye amani, maendeleo na ustawi kwa wananchi wake.