Watu 90,000 walazwa nchini Marekani kwa kuambukizwa COVID-19
2020-11-27 08:57:49| CRI

Shirika la kujitolea la kukusanya takwimu za COVID-19 nchini Marekani limesema, karibu watu 90,000 walioambukizwa virusi vya Corona wamelazwa hospitalini katika Siku ya Shukrani (Thanksgiving), na kuweka rekodi mpya kwa siku ya 16 mfululizo. Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC kimekadiria kuwa, idadi ya vifo vinavyotokana na janga hilo huenda itaongezeka ndani ya wiki nne zijazo. Kituo hicho kilitoa mwongozo mpya Ijumaa iliyopita kikiwataka wamarekani kukaa nyumbani na kutowatembelea ndugu, jamaa na marafiki katika Siku hiyo.