Rais wa Guinea ya Ikweta kuhudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali mpya itakayojengwa kwa msaada wa China
2020-12-01 18:24:43| cri

Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema amehudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali mpya itakayojengwa kwa msaada wa China, na kusema mradi huo ni matunda mengine ya ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.

Katika hotuba yake, rais Obiang Nguema amesema, pande hizo mbili zitajitahidi kwa pamoja kukabiliana na athari zinazotokana na janga la virusi vya Corona na kusukuma mbele utelekezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake, balozi wa China nchini Guinea ya Ikweta Bibi Qi Mei amesema, China inapenda kuendelea kushirikiana na Guinea ya Ikweta katika kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa pande hizo mbili, kuunganisha mikakati ya maendeleo, na kusukuma mbele ushirikiano wa nchi hizo mbili ufikie ngazi ya juu zaidi.