Chombo cha anga ya juu cha China Chang’e-5 chamaliza kukusanya sampuli kutoka Mwezini
2020-12-03 18:32:21| CRI

Chombo cha anga ya juu cha China Chang’e-5 chamaliza kukusanya sampuli kutoka Mwezini

Chombo cha anga ya juu cha China Chang’e-5 kimemaliza kukusanya sampuli Mwezini, na sampuli hizo zimefungwa na kuhifadhiwa ndani ya chombo hicho.

Idara ya Taifa ya Anga ya Juu ya China imesema, baada ya kufanya kazi kwa saa 19 Mwezini, ukusanyaji wa sampuli hizo ulikamilika saa nne usiku jumatano kwa saa za Beijing.

Kwa kutumia data zilizotumwa na chombo hicho, watafiti waliigiza mchakato wa ukusanyaji wa sampuli katika maabara, na kutoa msingi muhimu kwa operesheni hiyo ya Mwezini.