Kamishna msaidizi wa Mamlaka ya Hifadhi ya kitaifa ya Tanzania TANAPA Bw. Paul Banga, amesema serikali ya Tanzania imeidhinisha mamlaka hiyo kuweka vigari vya kebo katika Mlima Kilimanjaro. Amesema vigari hivyo vitawekwa hadi kwenye urefu wa mita 3,700 kwenye mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.