Mwanamume amaliza supu ya moto kuepuka kulipa mahari kubwa
2020-12-21 10:30:34| cri

Mwanaume mmoja na mchumba wake walikuwa wakila chakula cha jioni kwenye mgahawa wa hotpot huko Tianshui, mkoani Gansu, wakati walipozungumzia suala la mahari. Mwanamume huyo alimwambia mchumba wake yuan 200,000, sawa na dola elfu 30 za kimarekani, ni nyingi sana, na kwamba yeye hachumi pesa nyingi, na hana njia ya kubana matumizi ya pesa kiasi hicho. Mchumba wake alimtaka aombe msaada kwa wazazi wake. Lakini mwanaume huyo alijibu kuwa, pesa za wazazi wake ni zao wenyewe na si zake, kwa hivyo hawezi kuzitumia kama mahari. Wakati huo mchumba wake alipoteza uvumilivu akisema, hili ni suala kuhusu ndoa, si kama mtu anayenunua mboga sokoni. Mwanamume huyo alitaka kumsihi mpenzi wake, lakini alishindwa. Na mwanamke huyo alisema kama mwanaume akimaliza supu moto ya hotpot, basi ataweza kuacha matakwa yao ya mahari. Mwanaume huyo aliposikia haya, alijibu ikiwa hii ndivyo anayotaka atafanya hivyo, na akamaliza kunywa supu moto.

Kwa tukio hilo, baadhi ya wanamtandao wamemhurumia mwanaume wakiona kuwa haifai kupoteza wakati kwa kuishi na mwanamke kama huyo. Ndoa ni jambo ya upendo, na si biashara. Wengine wanamhurumia mwanamke, wakisema kama mwanaume hataki kulipa mahari, je, upendo wake ni wa kweli? Hata wakioana mwanamke hatakuwa na furaha.