1222 China yaimarisha usimamizi juu ya elimu baada ya masomo shuleni
2020-12-16 14:39:38| cri

Ofisa wa Wizara ya Elimu ya China Xu Pan amesema, China itachukua hatua zaidi kusimamia na kuelekeza maendeleo ya elimu baada ya masomo shuleni. Amesema wizara hiyo itashirikiana na mamlaka nyingine kufanya ukaguzi wa mara kwa mara juu ya mashirika ya mafunzo nje ya shule, na kwamba shule zote zimehimizwa kutoa elimu bora, na mipango ya elimu baada ya masomo ya shuleni. 

Mashirika ya mafunzo nje ya shule pia yameagizwa kutolenga kutafuta faida za kiuchumi tu, na kuhamasisha hatari kwa wazazi.

Katika miaka miwili iliyopita, China imekuwa ikiimarisha kanuni zake za elimu baada ya masomo ya shuleni, ambapo utaratibu wa usimamizi wa muda mrefu umeanzishwa na mashirika ya mafunzo yameagizwa kuboresha huduma zao ili kufikia vigezo vinavyotakiwa.