Je, wanawake kununua nyumba kunamaanisha wanajitegemea?
2020-12-21 18:44:56| cri

Hivi karibuni suala la “wanawake wanaonunua nyumba” ambalo lilijadiliwa kwenye kipindi cha televisheni linafuatiliwa sana na watu.  Baadhi ya watu wanaona hali hii inaonesha kujitegemea kwa wanawake. Lakini Je, uhuru wa wanawake lazima utegemee mali yenye thamani kubwa kama nyumba?

 

Tukiwaangalia wanawake ambao tayari wamenunua nyumba zao wenyewe, tunaweza kugundua wanajiamini zaidi katika masuala yanayohusiana na ndoa au uhusiano wa kimapenzi. Kwa wanawake, kununua mali zao wenyewe kunawasaidia kujenga imani na kupunguza hatari yao ya kudhibitiwa na wanaume.

Lakini kwa upande mwingine, pia tunapaswa kuona kuwa “wanawake kununua nyumba” hakuwezi kulinganishwa tu “uhuru wa wanawake”, kwani mtu anayemiliki mali, haimaanishi kuwa amefanya uamuzi huru kwa kujitegemea. Zaidi ya hayo, mwanamke wasio na uwezo au nia ya kununua nyumba, hakumaanishi kuwa amekosa tiketi ya kuwa “mwanamke huru”. Kwani umiliki wa mali sio njia mwafaka ya kutathmini uhuru wa mtu.