Msichana wa Sichuan aliyeambukizwa COVID-19 asuthumiwa vilani na wanamtandao
2020-12-23 18:40:04| cri

Hivi karibuni msichana mwenye umri wa miaka 20 mkoani Sichuan alishutumiwa vikali na wanamtandao kutokana na kutangazwa kwa picha ya ratiba ya usafiri wake kwenye mtandao wa Internet. Picha hii imeonesha kuwa alikwenda sehemu nyingi kabla ya kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, ambapo aliwatembelea babu na nyanya yake, wazazi, alikwenda saluni ya ukucha, mikahawa na baa kadhaa.

Baada ya hapo, vurumai kuwa ilizuka kwenye mtandao, si kama tu wanamtandao walipata jina lake, nambari yake ya kitambulisho chake, ilipo nyumba yaje, uhusiano wa kifamilia, baadhi yao pia walianza kumchafua mtandaoni na kumdhihaki. Watu wengine walisema ingawa alikuwa anajua kuwa bibi yake alikuwa amethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, yeye alikuwa anazurura bila kujali. Lakini ukweli ni kwamba, bado haijulikani kama alikuwa anajua kuwa bibi yake alikuwa ameambukizwa virusi au la.

Lengo la serikali kutangaza aliposafiri mgonjwa ni kuwawezesha wananchi kufahamu wakati uwezekano wa kuambukizwa kwao, wala si kuingilia faragha ya wagonjwa. Bahati mbaya ni kuwa, katika zama ya mitandao, uvumi unaenea kwa kasi kuliko ukweli. Watu wengi zaidi wanadhuru faragha ya watu, na kuchochea vurugu za kimtandao.