1223 Je matokeo ya mtihani ya wanafunzi yanatakiwa kutangazwa hadharani?
2020-12-23 10:30:06| cri

Hivi karibuni shule nyingi mjini Hangzhou zimeanza kutekeleza kanuni kuhusu kutoruhusu walimu kutangaza wazi matokeo ya mtihani kwenye mtandao wa kijamii wa Wechat, ili kulinda faragha ya wanafunzi. Hatua hii imezusha mjadala mkubwa.

Mkoa wa Guangdong pia umetangaza kanuni kama hii, lakini walimu wanaweza kuwasiliana na wazazi kuhusu hali ya masomo ya wanafunzi. Wataalamu wameeleza kuwa, wazazi hawapaswi kuzingatia tu matokeo ya mtihani, bali wanatakiwa kufuatilia hali ya jumla ya ukuaji wa watoto.

Baadhi ya wanamtandao wanaona kuwa kanuni hii inasaidia kulinda faragha ya wanafunzi. Lengo la shule ni kuzuia wanafunzi kushindana darasani, ili kupunguza shinikizo lao. Lakini wengine wanaipinga wakisema, ni wazazi tu wanaotumia mtandao wa kijamii, na kutangazwa kwa matokeo ya mtihani hakutaathiri wanafunzi. Na kutangaza wazi matokeo ya mtihani kutawasaidia wanafunzi kufahamu nafasi zao za masomo darasani, ili kuwahamasisha wasome kwa bidii.