Mkoa wa Yunnan: Atakayemficha ukweli mwenzi wake kuhusu maambukizi ya VVU atafunguliwa mashtaka ya kosa la jinai
2020-12-23 18:40:45| cri

Hivi karibuni mkutano wa 21 wa kamati ya kudumu ya bunge la awamu ya 13 la mkoa wa Yunnan umepitisha kanuni ya udhibiti wa UKIMWI ya mkoa huo, ambayo itatekelezwa rasmi kuanzia Machi Mosi mwaka kesho.

Kanuni hiyo imeweka bayana kuwa watu walioambukizwa VVU na wanaoishi na UKIMWI wanatakiwa kuwaambia ukweli wenzi wao wa ndoa au wapenzi wao kuhusu hali yao ya maambukizi, ambaye hatasema ukweli kuhusu hali yake kiafya, idara za afya zina haki ya kufanya hivyo. Kanuni hiyo pia inasisitiza kuwa yeyote aliyeambukizwa VVU na hatawajulisha kwa wakati mwenzi wake wa ndoa au mpenzi wake kuhusu maambukizi yake, atafunguliwa mashtaka kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Jinai.