Ombi la talaka la mwanamke aliyevumilia udhalilishaji wa ndoa kwa miaka 40 lakataliwa na mahakama
2020-12-23 18:38:54| cri

Mwanamke mmoja alitoa ombi la talaka baada ya kuvumilia udhalilishaji wa muda wa miaka 40 kwenye ndoa yake, lakini ombi lake lilikataliwa na mahakama ambayo inamsihi athamini maisha ya uzeeni yenye furaha.

Hivi karibuni tovuti ya Hati za Hukumu ya China imetangaza uamuzi juu ya mzozo mmoja wa talaka, ukisema mwanamke mmoja wa Mkoa wa Shaanxi amekuwa akipigwa na mumewe mara kwa mara katika miaka 40 iliyopita, na ilimbidi aombe talaka baada ya kuona watoto wake watatu wamekua watu wazima. Mahakama ilishikilia kuwa wanandoa hao wawili wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 40, na wanapaswa kuthamini uzee wenye furaha usiopatikana kwa urahisi, na kuishi pamoja kwa kusameheana.

 

Mume wa mwanamke huyo Bw. Yang hakukubali kutoa talaka, akisema ingawa alifanya makosa lakini alikuwa mwaminifu katika ndoa. Kwa maoni yake, wazee wanatakiwa kutunzana, na kutumai kuwa mke wake atampa fursa nyingine ili ajikosee.