Dereva wa Taksi apunguziwa alama 18 kutokana na kuvuka taa nyekundu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtoto
2020-12-23 18:41:26| cri

Dereva Taxi Bw. Ai kutoka mji wa Dongguan mkoani Guangdong hivi karibuni alipokea oda ya huduma ya Texi kupitia mtandao, na abiria walikuwa ni wanandoa pamoja na mtoto wao mchanga, lakini muda mfupi baada ya kupanda gari lake, mtoto huyo akapoteza fahamu ghafla kutokana na ugonjwa.

Ili kuokoa maisha ya mtoto huyo, Bw. Ai alivuka taa nyekundu mara tatu wakati akimkimbiza mtoto huyo hospitali. Kutokana na makosa yake hayo, dareva huyo alipunguziwa alama 18, na kutozwa faini ya yuan 600. (Nchini China kila dereva mwenye leseni ana alama 12 kila mwaka, atapunguziwa alama mbili hadi sita kutokana na makosa anayofanya barabarani, na atafutiwa leseni yake kama alama zote 12 zikitolewa ndani ya mwaka mmoja.) Polisi wa usalama barabarani wamesema, Bw. Ai alifanya makosa hayo katika hali ya dharura ya kuokoa maisha, na kama akitaka kufutiwa adhabu, ni lazima awasilishe hati za uthibitisho zinazotolewa na hospitali. Lakini jambo linaloshangaza ni kwamba wazazi wa mtoto huyo walikataa kutoa ushahidi na kudai kuwa makosa ya dereva huyo hayahusiani nao.

Bw. Ai alisema abiria hao walikataa kupokea simu yake na pia kukataa kutoa ushirikiano, na walisema hawakumwambia kuvuka taa nyekundu.

Polisi wamesema dereva Ai atapunguziwa alama 18 kutokana na kuvuka taa nyekundu mara tatu, pamoja na kutozwa faini ya Yuan 600, pia atatakiwa kufanya upya mitihani ya leseni ya kuendesha gari. Bw. Ai akiwa ni derava Teksi, adhabu hizo zitamletea hasara kubwa. Hivi sasa Polisi wameanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, Bw. Ai amesema ingawa majibu ya wazazi wa mtoto huyo yalimvunja moyo, lakini hajutii kamwe kufanya hivyo ili kuokoa maisha ya mtoto.