Aina mpya ya ndoa yaibuka nchini China
2020-12-25 19:55:29| cri

Katika miaka ya hivi karibuni, aina mpya ya ndoa imeibuka katika baadhi ya sehemu nchini China. Kwa aina hiyo ya ndoa, baada ya kuoana, pande mbili za wanandoa wanaishi na familia ya upande wa mume au mke kwa muda fulani unaoamuliwa baada ya kujadiliana kwa pande mbili za wanandoa. Kwa kawaida kama wana watoto wawili, mmoja anapewa jina la ukoo upande wa baba, ambaye anakua kwa kutegemea zaidi upande wa baba; mwingine anapewa jina la ukoo upande wa mama, na kukua kwa kutegemea zaidi upande wa mama.

Mwanasheria wa Kampuni ya Sheria ya Siwei ya Mkoa wa Zhejiang Bibi Yang Hong anaona familia ya aina hiyo inakubali kuwa na watoto wawili, hali ambayo ni mwitikio mzuri kwa sera ya uzazi ya China, na kupunguza matatizo yanayotokana na ongezeko la idadi ya wazee katika jamii. Vilevile hakuna tatizo la mahari, na shinikizo la kiuchumi kwa pande zote mbili za mwanamume na mwanamke pia linapungua. Zaidi ya hayo, watoto wawili wanafuata majina ya baba na mama, hali ambayo imeepusha mabishano juu ya majina na malezi.   

Lakini pia kuna matatizo mengi katika ndoa aina hiyo, ambayo yanafuatiliwa na watu. Kwa mfano, wanandoa wanawezaje kuhakikisha ukamilifu wa ndoa yao? Je, ndoa aina hiyo itaathiri uhusiano kati ya wanandoa au la? Watoto wawili wakilelewa kwa kutengana, kunaweza kutaleta matatizo ya matunzo?