China imefanikiwa kurusha satelaiti mpya ya uchunguzi wa dunia kutoka kituo cha kurushia satelaiti cha Jiuquan, kaskazini magharibi mwa China jana usiku.
Satelaiti hiyo ya Yaogan-33 iliyorushwa kwa kutumia roketi ya Long March-4C, imeingia kwenye obiti kama ilivyopangwa, na itatumika kwenye majaribio ya kisayansi, uchunguzi wa raslimali za ardhi, makadirio ya uzalishaji wa kilimo na pia kuzuia maafa.