China yafanya vizuri zaidi kwenye kupunguza changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kuliko ilivyotarajiwa
2020-12-29 14:32:59| cri

Wakati tunamaliza mwaka wa 2020 kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo wengi tutayakumbuka. Makubwa mawili ni maambukizi ya virusi vya Corona na changuzi mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa Marekani ambapo wamarekani wamemwondoa madarakani Bw. Donald Trump kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Novemba.

Kuna mengine ambayo yamegusa watu wote duniani, moja ikiwa ni lile linalohusiana na mabadiliko ya tabia nchi. Ambapo China imetajwa kuwa imefanya vizuri kwenye kupunguza utoaji wa hewa ya Carbon kuliko iliyotarajiwa, na katika mwaka 2020 China imepata maendeleo makubwa kwenye matumizi ya nishati endelevu, matumizi ya nishati ya nyuklia, upandaji wa miti kwenye kinachoitwa na wataalamu kuwa ni “carbon capture”.

Kulikuwa na mengine kwenye sekta ya michezo na burudani. ikiwa ni pamoja na vifo mbalimbali, kama vile kifo cha mcheza mpira wa kikapu Kobe Bryant, mcheza soka Diego Maradona. Vifo ambavyo viliwagusa wapenzi wa michezo katika nchi mbalimbali duniani.

Lakini pia kwenye sekta ya habari kulikuwa na changamoto kubwa kuliko wakati wowote ule. Habari zinazopata kwenye vyombo vya jadi vya habari zilishambuliwa na baadhi ya wanasiasa na kuitwa “fake news” na habari zisizo rasmi na zisizo na ukweli zilianza kuonekana kuwa ni habari za kweli.