Asilimia 80 ya wanafunzi warudi China baada ya kusoma nje ya nchi katika miaka mitano iliyopita
2020-12-30 15:09:45| cri

Hivi karibuni Wizara ya Elimu imefanya mkutano na waandishi wa habari. Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano na Mawasiliano ya Kimataifa kwenye Wizara ya Elimu Bw. Liu Jin ameeleza kuwa, kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, watu milioni 2.518 walisoma nje ya nchi, na milioni 2.013 walirudi China, ikiwa ni karibu asilimia 80. Waraka umeonesha kuwa watu waliosoma nje ya nchi na kurudi China wana faida dhahiri katika kupata ajira.

Mwaka 2018, asilimia 59 ya wahojiwa walisema, “kuwa na mtazamo wa kimataifa” ni moja kati ya sifa kubwa kwa wanafunzi waliosoma nje ya nchi na kurudi China, na kiwango hicho kiliongezeka hadi asilimia 68 mwaka 2019.  Sifa inayofuata ni “ Ustadi katika uwezo wa lugha”.

Katika utafiti wa Waraka wa mwaka 2020 kuhusu wanafunzi wa China waliosoma nje ya nchi, asilimia 61 ya wahojiwa walisema, walichagua kurudi nchini China kupata ajira, asilimia 5 walichagua kuanzisha biashara nchini China, na wengine wapatao theluthi moja ya watu walichagua njia nyingine, ikiwa ni pamoja na kutafuta ajira, kuendelea na masomo au kufanya mapumziko kwa muda.

Wanafunzi walisoma nje ya nchi na kurudi nchini China wanapewa ajira katika sekta mbalimbali, na wengi kati yao wanashughulikia mambo ya IT, mawasiliano, elektroniki na mtandao wa Internet.

Takwimu zimeonesha kuwa wastani wa mshahara wa watu hao ni karibu yuan 10,996, sawa na dola za kimarekani 1681, ambayo imezidi kwa dola za kimarekani 382 kuliko mshahara wa wastani kote nchini.