China yapunguza umri wa chini wa kuwajibika kwa makosa ya jinai hadi kufikia miaka 12
2020-12-30 15:11:20| cri

Hivi karibuni mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China ulipitisha mswada wa marekebisho ya 11 ya sheria ya makosa ya jinai, ambao umepunguza umri wa chini wa kuwajibika kwa makosa ya jinai hadi kufikia miaka 12. Kwa mujibu wa muswada huo, vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14 waliokutwa na hatia ya mauaji ya kukusudia, hawatakuwa na kinga ya kutowajibika na makosa yao. Watoto wenye umri chini ya kikomo hicho waliotenda makosa ya jinai hawatapewa adhabu kulingana na sheria ya makosa ya jinai, lakini watapewa mafunzo maalumu ya kurekebisha tabia, baada ya kufanyiwa tathmini na kuidhinishwa na Kamati ya elimu maalumu.