Viongozi wa China na nchi za Ulaya watangaza kukamilisha mazungumzo kuhusu mkataba wa uwekezaji kwa wakati uliopangwa
2020-12-31 09:59:50| CRI

Viongozi wa China na nchi za Ulaya watangaza kukamilisha mazungumzo kuhusu mkataba wa uwekezaji kwa wakati uliopangwa_fororder_1126929248_16093439963981n

Viongozi wa China na nchi za Ulaya watangaza kukamilisha mazungumzo kuhusu mkataba wa uwekezaji kwa wakati uliopangwa_fororder_1126929248_16093439964031n

Rais Xi Jinping wa China jana usiku hapa Beijing alifanya mazungumzo na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, mwenyekiti wa baraza la Ulaya Bw. Michel Barnier na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen kwa njia ya video. Viongozi hao walitangaza kwa pamoja kukamilisha mazungumzo kuhusu mkataba wa uwekezaji (BIT) kati ya China na Ulaya kwa wakati uliopangwa.

Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa China inafanya juhudi kujenga muundo mpya wa maendeleo na itatoa fursa nyingi zaidi za soko na kuweka mazingira makubwa zaidi ya ushirikiano kwa Ulaya na dunia. Amezitaka nchi za Ulaya zishikilie sera ya biashara huria na mfumo wa pande nyingi, na kuweka mazingira ya kibiashara yenye uwazi, haki na bila ubaguzi kwa wawekezaji wa China.