Vifo vya ghafla vya wafanyakazi wa kampuni za mtandao chazusha mjadala kwenye jamii
2021-01-07 16:36:30| cri

Hivi karibuni mfanyakazi mwanamke mwenye umri wa miaka 23 wa kampuni ya biashara ya mtandaoni alifariki ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kazi katika muda wa ziada mpaka saa saba usiku. Desemba 4 mwaka jana mfanyakazi mwingine wenye umri wa miaka 27 wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Gome tawi la mji wa Fuzhou alifariki ghafla kwenye mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, na uchunguzi wa kimatibabu unaonesha kuwa alifariki kwa kufanya kazi kupita kiasi. Mwezi Aprili mwaka 2017, msanifu mwingine mwenye umri wa miaka 27 alifariki dunia wakati akiwa kazini kwa muda wa ziada.

Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka watu wapatao laki 5.5 nchini China wanakufa ghafla kutokana na matatizo ya moyo, ikiwa ni wastani wa zaidi ya watu elfu moja kwa siku. Vifo hivyo vya ghafla vya vijana vimezusha mjadala mkubwa kwenye jamii, kuhusu kundi la vijana kukabiliwa na shinikizo kubwa kiasi cha kusababisha vifo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, dhana ya kifo cha ghafla ni watu wenye hali nzuri ya afya au wanaoonekana kuwa na afya nzuri kufariki ndani ya muda mfupi kutokana na magonjwa. Dhana hiyo inaonesha kuwa kifo cha ghafla hutokana na magonjwa au sababu za kiafya, lakini kama tunavyojua, kufanya kazi kupita kiasi, shinikizo kubwa linalotokana na kazi, na mienendo mibaya ya maisha pia vinaleta madhara makubwa kiafya.

Wakati Wanamtandao wa China wanazilaani kampuni za mtandao kuwalazimisha wafanyakazi wao kufanya kazi kupita kiasi, pia wanajiuliza kwamba ni kweli vijana wanastahili kufanya kazi kwa bidii kiasi cha kudhuru afya zao.