Mzee aliyepooza aoga baada ya kupata huduma ya kuogesha watu wenye matatizo
2021-01-07 16:35:20| cri

Inawezekana mtu akaishi miaka 11 bila kuoga? Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza。Ingawa kuoga ni jambo dogo, lakini si rahisi kwa wazee wenye matatizo ya kutembea.

Wasaidizi wanne walimzunguka mzee Yao kumbadilisha nguo zake nzito, pajama, soksi na kisha kumfunika na kitambaa cha kuoga, huku yeye mwenyewe akiwa amelala vizuri kwenye kitanda kimoja karibu na roshani. Mkewe Zhang Zhengying alikuwa ameegemea mlango wa chumba, akiongea na wasaidizi mara kwa mara: “Soksi ziko chini ya kitanda… Hili ni taulo safi, lile jeupe ni la kufutia uso… miguu yake imepooza, msiifanye atumie nguvu…”

Utoaji wa huduma za kuwasaidia watu kuoga nyumbani ulianzishwa nchini Japan. Wasaidizi wanaleta bafu la kukunjwa, safu ya vyoo, na mbinu salama za kuwaogesha wazee. Inachukua saa moja hadi mbili kutoa huduma za kuogesha. Kwa wazee wenye matatizo ya akili au walemavu ambao hawawezi kuoga kwa miaka mingi, kuna umuhimu mkubwa kwa wao kuwa na huduma kama hii.