Wafanya biashara wa Uganda wataka ujenzi wa soko umalizike haraka
2021-01-08 16:35:20| cri

Wafanya biashara nchini Uganda wameonyesha hofu yao kufuatia kucheleweshwa kwa kumalizika kwa ujenzi wa soko la Kitooro na eneo la kuegesha magari katika manispaa ya Entebbe. Miaka miwili iliyopita, wafanya biashara hao waliondolewa kutoka kwa soko hilo ili kutoa nafasi ya ujenzi wa soko hilo. Jumla ya wafanya biashara 1000 walikuwa na matumaini kuwa ifikapo juni mwaka huu eneo la kuegesha magari ya texi pamoja na soko hilo yatakuwa yamekamilika na kufunguliwa rasmi. Wameongeza kuwa baadhi yao hawafanyi kazi hivi sasa kwa sababu hawana sehemu ya kufanyia biashara zao. Soko la Kitooro limekuwa likiwahudumia wakazi wa Entebbe kwa muda mrefu pamoja na wageni kutoka nchi jirani kama vile Kenya, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.Wafanya biashara wengi wa Uganda hununua bidhaa nyingi kutoka China na kuwauzia wateja wao kutoka eneo zima la Afrika mashariki.