TABLE TENNIS: Meza Taifa wakabidhi mpango mkakati BMT
2021-01-08 15:35:28| cri

Uongozi wa Chama cha Mpira wa Meza Tanzania (TTTA) umekamilisha na kukabidhi Mpango mkakati na kalenda ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Michezo (BMT). Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Chama hicho, Yahya Villu, alisema mpango mkakati huo, umeainisha mipango ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mwaka huu. Alisema wanakusudia kuwa na mashindano mengi ya ndani ili kuwapa uzoefu na kupima viwango vya wachezaji kwa kushiriki zaidi mafunzo ya uwamuzi na ukocha. Villu alisema kimataifa wanatarajia kuandaa mashindano mawili pekee mwaka huu yaliyowekwa kwenye kalenda, kwani walibaini kuwa wachezaji hawana uzoefu wa kushiriki mashindano, hivyo wanajipanga upya kwa mashindano ya kimataifa yajayo.