Mradi wa kuboresha maeneo ya usafiri katika uwanja wa Jomo Kenyatta waanza rasmi
2021-01-08 16:34:34| cri

Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Kenya KAA imeanza mradi wa kufanyia marekebisho uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma kwa wasafiri. Mradi huo utakaogharimu jumla ya shilingi milioni 963 unalenga maeneo ya kufanyiwa ukaguzi kabla ya kusafiri kwa ajili ya kuboresha huduma za ukaguzi wa stakabadhi, usalama na sehemu ya wasafiri kupumzika wakisubiri usafiri wao. Kufuatia marekebisho hayo  wasafiri sasa watatakiwa kufika katika uwanja wa ndege saa nne kabla ya muda wa usafiri. Ndege ambazo zimekuwa zikitumia maeneo hayo zimehamishiwa maeneo mengine ili kutoa nafasi kwa marekebisho hayo.  Meneja mkuu wa KAA Alex Gitari amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi za kutimiza matakwa ya wasafiri pamoja na wadau kwenye sekta hiyo ya usafiri.