SOKA: Azam FC kumenyana na Yanga nusu fainali kombe la Mapinduzi
2021-01-11 17:02:00| CRI

Nahodha wa Klabu ya Azam FC, ambaye ni beki mkongwe Agrey Moris dakika ya 62 amepachika bao la ushindi mbele ya Malindi kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi.  Azam FC imeshinda bao 1-0 Uwanja wa Amaan na kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuwa inaongoza kundi C na pointi zake nne. Mabingwa hao mara tano wa Kombe la Mapinduzi, leo watakutana na Yanga ambao ni vinara wa kundi A nao wakiwa na pointi nne na wamefunga bao moja huku Azam FC ikiwa imefunga mabao mawili. Nusu fainali nyingine ni dhidi ya Simba ambao watamenyana na Namungo ambao hawa ni best looser wakiwa na mabao mengi ambayo ni mawili na pointi zao ni tatu kama ilivyo kwa Mtibwa Sugar ambao walivuliwa ubingwa na Simba kwa kufungwa mabao 2-0.

Simba inaongoza kundi B ikiwa na pointi sita imeshinda mechi zote mbili na ina mabao matano kibindoni, kinara wa kucheka na nyavu ni Miraji Athuman mwenye mabao matatu. Pia kinara wa pasi za mwisho ni David Kameta mwenye pasi mbili za mabao.