SOKA: Mauricio Pochettino asisitiza kikosi chake cha PSG kinapaswa kuongezeka ubora
2021-01-11 17:08:10| CRI

SOKA: Mauricio Pochettino asisitiza kikosi chake cha PSG kinapaswa kuongezeka ubora_fororder_csportfotomauricio-pochettino

Kocha Mauricio Pochettino amesisitiza kwamba kikosi chake kinapaswa kuongezeka ubora baada ya timu yake mpya ya Paris Saint-Germain kushinda 3-0 dhidi ya Brest juzi Jumamosi. Wakitokea benchini Mauro Icardi na Pablo Sarabia waliongeza mabao juu ya lile alilotangulia kufunga Moise Kean wakati mabingwa watetezi hao wakipata ushindi wa kwanza chini ya kocha Pochettino. Ushindi huo umekuja siku tatu tangu sare ya 1-1 dhidi ya SaintEtienne katika mechi ya kwanza ya Pochettino madarakani, na kuipandisha PSG hadi pointi moja nyuma ya vinara Lyon, ambao walishikiliwa kwa sare ya 2-2 dhidi ya Rennes. Alisema wameridhishwa na ushindi, lakini kuna mengi ya kurekebisha.