Tanzania imesaini kandarasi ya dalo bilioni 1.32 msaada kutoka China
2021-01-11 19:05:53| CRI

Tanzania imesaini kandarasi ya dalo bilioni 1.32 msaada kutoka China  kwa ujenzi unaoendelea wa reli ya kawaida.

Rais John Magufuli amesaini kandarasi hiyo  na Waziri wa Mambo ya nje wa China Wang Yi ambaye amekuwa kwenye ziara ya muda mfupi.

Mchangao huo utashughulikia ujenzi wa reli ya 341km kati ya Mwanza na bandari kavu ya Isaka.

Katika makubaliano hayo, kampuni mbili za china ambazo ni The China Civil Engineering Construction and China Railway Construction Company,  zitachukua mradi huo.

Waziri wa China pia aliahidi $ 150,000 kusaidia upanuzi wa kituo cha mafunzo ya ufundi katika mji wa Rais Magufuli wa Chato, na dola nyingine 20,000 kukuza shughuli za uvuvi katika ukanda wa Ziwa Victoria.

Tanzania inaangalia kuingia katika soko kuu la China kupitia biashara za uagizaji na mauzo ya nje.