Kenya Kampuni kadhaa za kilimo cha bustani zimeondoka Kaunti ya Narok baada ya serikali ya mkoa kuweka ushuru
2021-01-11 19:06:29| CRI

Kampuni kadhaa za kilimo cha bustani zimeondoka Kaunti ya Narok baada ya serikali ya mkoa kuweka ushuru wa Sh100 kwa kreti ya maharagwe ambayo yanazalishwa huko.

Kaunti ilianzisha ushuru kupitia bili yake ya kifedha hivi karibuni, ikiongeza gharama ya kitengo cha uzalishaji wa zao hilo huko Narok.

Kampuni ambazo zilikuwazinakodisha ardhi kwa ajili ya kilimo hicho, ambazo tarayi zimejitoa zimesema kuwa kaunti hazipaswi kulazimisha ushuru mwingi kwa mazao ya kilimo kwani hatua hiyo itawavunja moyo wawekezaji kufanya biashara katika mikoa yao.

Ushuru mkubwa haujaathiri wawekezaji wa maharagwe ya Ufaransa peke yao.

Kumekuwa na visa vya kampuni za maua kufunga kampuni zao nchini Kenya na kuhamia Ethiopia katika siku za hivi karibuni juu ya ushuru kuongezwa mara dufu na kaunti.