Takwimu za bei ya vyakula kutoka FAO zinaonesha bei ya chakula ulimwenguni ilipanda kwa miezi saba mfululizo
2021-01-11 19:05:22| CRI

Takwimu za bei ya vyakula zilizotolewa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, zinaonesha bei ya chakula ulimwenguni ilipanda kwa miezi saba mfululizo hadi mwezi  Desemba mwaka jana, ikiongozwa na bidhaa za maziwa na mafuta ya mbogamboga.

Bei ya kuuza nje ngano, mahindi, mtama na mchele vyote vilipanda mnamo Desemba, bei zikipanda juu kwa sehemu fulani kwa sababu ya wasiwasi juu ya hali ya ukuaji na  matarajio ya mazao huko Amerika Kaskazini na Kusini na Urusi. Kwa mwaka, bei za kuuza nje mchele zilikuwa asilimia 8.6 juu katika mwaka 2020 kuliko mwaka 2019, wakati zile za mahindi na ngano zilikuwa asilimia 7.6 na asilimia 5.6 juu, mtawaliwa.

FAO inasema bei ya mafuta ya mboga iliongeza asilimia 4.7 mnamo Desemba kufikia kiwango cha juu kabisa tangu Septemba 2012

Kwa upande wa bidhaa za maziwa, FAO inaonesha bei zilipanda kwa asilimia 3.2 mwezi Desemba ikiwa ni ongezeko mfululizo kwa miezi saba. 

Kwa upande wa nyama, bei ziliongezeka kwa asilimia 1.7 ikilinganishwa na katika mwaka uliokuwa umetangulia yaani 2019 ambapo kiwango cha juu bei ilipanda kwa asilimia 4.5. 

Kiwango cha bei ya sukari kwa mujibu wa FAO kilipungua kwa asilimia 0.6 mnamo Desemba mwaka jana baada ya ongezeko kubwa wakati wa mwezi Novemba. Kwa mwaka 2020 kwa ujumla, ongezeko lilikuwa asilimia 1.1 juu kuliko mwaka 2019.