Mzee afukuzwa kutoka kwenye gari kutokana na kushindwa kuonesha namba ya afya
2021-01-12 12:26:09| cri

Tarehe 6 Januari, kwenye basi No. 85 ya mji wa Fushun, mkoani Liaoning, mzee mmoja alifukuzwa kutoka kwenye basi hilo kutokana na kushindwa kuonesha namba ya afya kwa kutumia simu ya mkononi. Video iliyosambazwa kwenye mtandao wa Internet imeonesha kuwa, mzee huyo alisema anaweza kujiandikisha kwenye kumbukumbu, lakini abiria wengine walipiga kelele wakisema “Usijiandikishe, Shuka!” Baada ya kujadiliana na dereva wa basi bila ya matokeo, mzee huyo alishuka.

Siku iliyofuata, Kampuni ya Mabasi ya Fushun ilijibu tuhuma kuhusu tukio hilo ikisema, kampuni hiyo imepokea taarifa kutoka Idara ya Usafirishaji kuwa, kuanzia tarehe 6, watu wote lazima wawe na nambari ya afya ya kupanda basi. Hakuna vikundi maalumu vinavyoweza kusamehewa, na pia hairuhusiwi kujiandikisha. Hivi sasa kampuni hiyo inaripoti matatizo mbalimbali katika mchakato huo, ikiwa ni pamoja na wazee ambao wanashindwa kuonesha namba ya afya.