Kocha mpya wa Gor Mahia apewa jukumu gumu kurudisha hadhi ya timu
2021-01-12 17:03:39| cri

Kocja Mkuu mpya wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya Carlos Manuel Vaz Pinto amekabidhiwa majukumu mazito ili kurejesha hadhi ya klabu hiyo katika kiwango bora kwa kuiongoza kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Makamu wa mwenyejiti wa klabu hiyo, Francis Wasuna, amesema Pinto mwenye leseni ya ukocha ya UEFA, amepewa mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo, akichukua mikoba ya Mbrazil Roberto Oliveira aliyeondoka katika klabu hiyo Desemba baada ya kushindwa kuleta mataokeo. Mabingwa hao wa Kenya walimuazima kocha wa Posta Sammy "Pamzo' Omollo aliyewasaidia wakati wa raundi ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati kocha msaidizi wazamani Patrick Odhiambo alikuwa akiisimamia timu hiyo katika mechi za ligi. Gor ilitolewa kwa aibu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 8-1 katika raundi ya kwanza dhidi ya mabingwa wa Algeria, CR Belouizdad katika raundi ya kwanza wiki iliyopita.