Wanadoa wazee wahukumiwa kifungo baada ya kukataa kugawa fidia ya kifo cha mwanao kwa mkwe
2021-01-12 12:10:28| cri

Wanandoa wazee wenye umri zaidi ya miaka 70 wanaoishi mjini Ya’an mkoani Sichuan, hivi karibuni wamepewa fidia ya Yuan milioni 1.2 na kampuni aliyofanya kazi mwanao kufuatia mtoto wao kufariki dunia akiwa kwenye safari za kikazi kutokana na ajali ya barabarani.

Mke wa marehemu Wang Qing anaona fidia hiyo inapaswa kuwa na gawio lake na pia la mtoto wake, lakini alipodai fedha hizo kwa baba na mama mkwe, alikataliwa na wazee hao. Baada ya madai yake kukataliwa mara nyingi, ili kupata fidia ya Yuan zaidi ya laki tisa aliyodai kuwa anastahili kupewa, Wang Qing aliwafungulia mashtaka ambayo mpaka sasa kesi yake imeendelea kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.

Disemba 5 mwaka 2019, makahama ya wilaya ya Shimian ilitoa hukumu kwa wazee hao kulipa gawio lao kwa Wang Qing na mtoto wake ndani ya siku kumi baada ya hukumu hiyo kutolewa, lakini walikataa tena kutekeleza hukumu hiyo ya mahakama.

Disemba 30 mwaka 2020, mahakama hiyo iliwahukumu wazee hao kifungo cha mwaka mmoja na miezi 10 na miaka miwili mtawalia, kutokana na kukataa kutekeleza hukumu ya mahakama.