Viongozi duniani watoa wito wa kuchukua hatua za pamoja kwenye anuai ya viumbe na mabadiliko ya tabia nchi
2021-01-12 18:49:04| CRI

Viongozi mbalimbali duniani jana walitilia mkazo haja ya kuchukua hatua za pamoja duniani ili kulinda uanuai wa viumbe na kwa ajili ya mfumo wa utawala duniani kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi baada ya janga la COVID-19.

Akihutubia viongozi wa dunia katika mkutano wa kilele wa Sayari Moja kwa ajili ya anuai ya viumbe, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema watu wamekuwa wakichafua hewa, ardhi na maji kwa sumu na kujaza plastiki kwenye bahari.

Ukiandaliwa na serikali ya Ufaransa kwa ushirikiano na UM na Benki ya Dunia, mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao, umewaleta pamoja viongozi wa dunia ili kuchukua hatua ya kulinda na kurejesha anuai ya viumbe.