Waethiopia wafanya vizuri kwenye mbio za Great Ethiopian Run, wakenya wabanwa
2021-01-12 17:02:44| cri

Wanariadha wa Ethiopia wameendeleza ubabe wao kwenye mbio za kilomita 10 za Great Ethiopian Run zilizofanyika Jumapili huko Addis Ababa. Abe Gashahun aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika 28:19.10, sekunde moja chini ya rekodi ya miaka 15 iliyowekwa na Deriba Merga. Ushindi huyo umemfanya Gashahun kuwa mwanariadha wa tatu baada ya Hagos Gebrhiwet (2012, 2018) na Azmeraw Bekele (2010, 2014) kutawazwa mfalme wa mbio hizo mara mbili. Wakenya wote waliokuwa wakishiriki makala ya 20 ya mbio hizo mwaka huu wa 2021 walitupwa nje ya mduara wa 20-bora. Tsigie Gebrselama aliyejipatia medali ya shaba katika Mbio za Nyika za Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2019, aliibuka mshindi wa kitengo cha wanawake baada ya kutumia muda wa dakika 32:33. Kennedy Kimutai, Solomon Boit na Evans Kipkemei waliokuwa wawakilishi wa Kenya waliambulia nafasi za 21, 27 na 35 mtawalia.