Yanga na Simba kukutana leo kwenye kombe la Mapinduzi Amaan Zanzibar
2021-01-12 17:03:18| cri

Baada ya kufanikiwa kuwachapa Azam kwa penati 5 kwa 4, Yanga imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Mapinduzi na leo inatarajiwa kukutana na Simba katika mchezo wa fainali utakaochezwa kwenye uwanja Amaan, Zanzibar. Yanga wawalitoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye mchezo uliochezwa jana jioni. Mabigwa wa Tanzania Bara, Simba SC nao pia wamefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja huo huo wa Amaan, Zanzibar jana usiku. Mabao ya Simba SC yalifungwa na washambuliaji wake Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya saba na Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika ya 41, wakati la namungo FC limefungwa na Mghana, Steven Sey katika dakika ya 88. Mechi ya fainali inachezwa leo usiku。 Hii inakuwa mara ya nane kwa Simba SC kuingia fainali ya michuano hiyo tangu ianzishwe mwaka 2007 wakiwa wametwaa Kombe hilo mara tatu.