WHO yafurahia kushirikiana na China katika chanjo na kutafuta chimbuko la virusi
2021-01-12 19:17:32| CRI

WHO yafurahia kushirikiana na China katika chanjo na kutafuta chimbuko la virusi_fororder_VCG111283663972

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Gebreyesus jana alisema anafurahi kwamba WHO inashirikiana na China katika chanjo ya COVID-19 na kutafuta chimbuko la virusi vya Corona. Pia amesema anatumai China itatoa chanjo ya COVID-19 yenye usalama na ufanisi haraka iwezekanavyo, na kuharakisha mchakato wa kugawanya kwa usawa kote duniani.

Bw. Tedros amesema jopo linaloundwa na wataalamu wa WHO  kutoka Australia, Danmark, Ujerumani, Kenya, Japan, Uholanzi, Qatar, Russia, Sudan, Uingereza, Marekani na Vietman limekuja China na kushirikiana na wenzao wa China kufanya utafiti wa kisayansi wa kutafuta chimbuko la virusi vya Corona.