Sudan Bajeti ya Kitaifa ya 2021 kusababisha kuporomoka kwa uchumi
2021-01-12 19:19:19| cri

Kamati ya Uchumi ya Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko (FFC) imeonya kuwa Bajeti ya Kitaifa ya 2021 iliyoidhinishwa na Baraza la Mawaziri wiki iliyopita itasababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi.

Kulingana na Kamati ya Uchumi ya FCC, bajeti ya ulinzi na usalama inapaswa kupunguzwa kwa angalau asilimia 40.

Bajeti iliyotengwa kwa elimu lazima iongezwe kwa angalau asilimia 50. Sekta ya miundombinu inapaswa kuwa na bajeti ya SDG milioni 6.

Mapato ya uchimbaji wa dhahabu na ushuru kwa kampuni zinazomilikiwa na jeshi na vifaa vya usalama hazijumuishwa kwenye bajeti.

Mchumi kutoka kwenye Kamati ya Uchumi ya FFC  alimtaka Waziri Mkuu Abdallah Hamdok kufanya kazi na bajeti iliyopita kwa muda mdogo mpaka uchunguzi wa Kamati ya Uchumi ya FFC uzingatiwe.

Wiki iliyopita, Kamati ya Uchumi ya FFC ilikabidhi hati kwa Waziri Mkuu Hamdok kuhusu "kukosekana kwa usawa mkubwa katika usambazaji wa rasilimali kati ya sekta mbali mbali nchini". Matumizi ya usalama, ulinzi, na polisi yaliwekwa kwenye SDG bilioni 245, wakati SDG 72 tu itatumika kwa afya, elimu, kilimo, uchukuzi, na miundombinu.